Jibu

Mungu anakualika kuwa sehemu ya hadithi ambayo anaandika kwa vizazi vitakavayokuja. Anakupa wokovu leo ambao ni mwaliko wako kwa wokovu ambao Mungu anakupa. Waweza kukumbatia wokovu wa Mungu kwa:

Kukubali unamuhitaji Mungu

Muombe akusamehe

Kumwamizi Yesu peke yake akuokoe

Kumfuata Yesu Kristo, Mfalme wa maisha yako, kwa imani kuanzia siku ya leo na zijazo

Wakati unapomwamini Yesu Kristo, unakuwa MWANA wa Mungu na roho wake anaanza kuishi ndani yako. Umekuwa sehemu ya hadithi yake. Unapozidi kukua katika uhusiano na Mungu, unazidi kuona na kuelewa hadithi yake maishani mwako. Dhambi zako zote, za zamani, za siku za usoni zimesamehewa na utapata kukubalika kabisa mbele zake. Unapoanza uhusiano huu, Yesu aahidi kuwa nawe kwa mazuri na mabaya na changamoto za maisha haya. Anakupenda na upendo usiobadilika wa milele. Na hajaahidi tu uzima wa milele, lakini alikuja ili uweze kukumbana na lengo, maazimio na uhuru wa maisha haya.

Sasa kwa sababu umeamini Yesu anyaye okoa, tungependa kukuombea na kukupa rasilimali zitakazo saidia ukuzaji wa imani yako:

NITAENDA WAPI KUTOKA HAPA?

Soma Bibilia

Bibilia ni hadithi ya upendo na uaminifu wa Mungu kwa watu wake.Inapeana himizo,maagizo,onyo na kukosoa ambao kutakusaidia kuboresha maisha yako. Unapokisoma,muulize Mungu akuonyeshe kitu unachoweza kuweka maishani mwako.Ikiwa hauna uhakika wa mahali pa kuanzia,aanza kwa kusoma kitabu cha Marko katika Agano jipya.

Kupata Jamii

Kuunganishwa na wengine ambao wameamini katika wokovu wa Mungu ni jambo la maana sana. Kanisa ni jamii ya wakristo ambao hukutana kila mara kumwabudu Mungu kama familia yake. Kila mmoja katika jamii ana jukumu; Jinsi ilivyo na mwili wa mwanadamu,kila sehemu inausaidia mwili wote kufanya kazi vizuri. Kanisa ni mwili wa Kristo.

Kuzungumza na Mungu

Kuzungumza na Mungu ni njia nyingine ya kumjua. Yuko tayari kila wakati kukusikiza na kuwa na wakati nawe, hivyo basi, waweza kuzungumza naye kila wakati. Anakualika umpatie mizigo yako yote na furaha yako; haya ni maombi.

Sema hadithi yako

Muambie kila mtu hadithi hii! Wacha wasikie kuhusu hadithi ya upendo na wokovu wa Mungu na jinsi umeyabadilisha maisha yako.

Uliza Swali

Skip to content