Kurasa zifuatazo ni muhtasari wa hadithi ya kweli. Ni kama hadithi nyingi nzuri ambazo umewahi kusikia au kusoma, lakini mara mingi unavyosoma, ndivyo jinsi unavayogundua kwamba sio tu hadithi nyingine-ni hadithi. Inatutambua sisi sote. Yatufanya kutafakari kuhusu sisi ni nani na nani twaweza kuwa. Na hivyo…

MUNGU

Hadithi yaanza na Mungu, ambaye amekuwapo. Amekuwepo tangu zamani na amekuwa jinsi alivyo sasa. Ikiwa yaonekana kama yachanganya, ni kwasabbau Yeye ni zaidi ya jinsi ambavyo mtu yeyote aweza kujua.

Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Zaburi 90:2 Kabla haijazaliwa milima,wala hujaiumba dunia,na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
UUMBAJI

Hapo mwanzo, Mungu alizungumza na kila kitu kikatokea. Kwa amri yake, ulimwengu wote uliumbwa na kujazwa na nyota na sayare-ikiwemo dunia ambayo ilikuwa na shamba zuri liitwalo Edeni. Katika urembo wote aliouumba, utaalamu wote ulikuwa ni mume na mke. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa kwa mfano wake ili wawe kielelezo chake. Waliumbwa na lengo kuu la kumwabudu kwa kumpenda, kumtumikia na kufurahia uhusiano wake na wao.

MAKUBALIANO

Kwa mpangilio wa Mungu,maumbile yote yalikuwa kwa umoja na kwa njiakamili ambayo ilipaswa kuwa.Wakati huu,machungu,mateso,magonjwa wala kifo havikuwepo. Kulikuwa na upendo,makubaliano na uhusiano wa karibu kati ya Mungu na mwanadamu,kati ya Adamu na Hawa na maumbile yote.Lakini,kitu kibaya kilifanyika…

KUTOTII

Adamu na Hawa hawangeweza kuwa sawa na Mungu ilhali aliwaweka kusimamia kila kitu alichokiumba katika bustani ya Edeni. Aliwapa uhuru wa kufanya maamuzi na kusimamia dunia kwa sheria moja;wasile tunda la mti Fulani. Siku moja,adui wa Mungu,malaika aliyenguka aitwaye Shetani alitaka kumpendua Mungu. Alichukua mfano wa nyoka na akawadanganya Adamu na Hawa. Aliwadanganya kufikiria ya kwamba Mungu sio mzuri na hakuwa na matakwa yao mazuri mawazoni mwake. Kutokana na haya,walikosa kumtii Mungu. Katika kuasi huku,Adamu na Hawa walikula lile tunda,wakaamua kwamba,wao na sio Mungu ndio watakaoamua kizuri na kibaya.

ATHARI

Athari ya matendo yao ni kali kabisa kama kirusi, dhambi iliingia katika maumbile yhote na kwa mioyo ya Adamu na Hawa. Dhambi, mateso na machungu yalienezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine; maumbile yote yaliharibiwa kutoka kwa hali yake ya kwanza. Sote tumesoma au kusikia hadithi za vita, umasikini, magonjwa, tamaa na vitu vibata ambavyo vimeukumba ulimwengu wa leo. Haya yote ni kutokana na dhambi.

Warumi 3:10 Hakuna mwenye haki,hata mmoja.
Warumi 3:19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati ili kila kinywa kifumbwe,na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu.
MAHITAJI

Tunapofikiria kuhusu ukamilifu na upendo uliokuweko mwanzoni mwa uumbaji, twagundua kwamba “tuna makosa mengi na dhambi kuliko tunavyoweza kudhania.” Hebu fikiria kuhusu visasi ambavyo tunavyo, uongo ambao tumesema, na mawazo ambayo hatujawahi kuyasema kwa sauti ya juu. Tunapojiangalia kwa undani mioyono mwetu, twaona ukweli; sote tu wakosaji. Kila mmoja ametenda dhambi na hatma ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko kifo cha mwili ni kutenganishwa milele kutoka kwa Mungu wa upendo katika hali ya machungu na huzuni. Kwasababu ya haya yote, twapaswa kuangazia maswali haya; Kuna jambo linaloweza kufanywa? Je, kuna tumaini yoyote?

AHADI YAFANYWA

Mungu aliwaondoa Adamu na Hawa kutoka kwa bustani ya Edeni kutokama na dhambi zao lakini aliwacha na ahadi ya kuwaokoa na tumaini. Aliwaahidi kwamba mmoja wa kizazi chao atakuja siku moja kuwaokoa wanadamu kutokana na dhambi. Kwa karne kadhaa zilizofuatia,Mungu alitayarisha njia ya mtu huyu ambaye angekuwa Mwokozi wa ulimwengu. Mambo kamili kuhusu kuzaliwa kwake,maisha na kifo yaliandikwa katika Bibilia karne nyingi kabla ya kuja kwake. Kwa hakika,Bibilia yaashiria mtu huyu mmoja kama lengo kuu la historia ya mwanadamu. Lengo kuu la kuja kwake ilikuwa “kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10).

AHADI YAWEKWA

Mwokozi aliyehadiwa alikuwa Mungu. Mungu alikuwa mwanadamu kupitia kwa Yesu Kristo takriban miaka elfu mbili iliyopita akitimiza utabiri wa Agano ya kale. Kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa kwa miujiza kwa vile mama yake alikuwa bikira. Maisha yake yalikuwa tofauti; Alifurahia na kumtii Mungu bila ya kutenda dhambi zozote. Mwishowe,mambo haya yalisababisha afe kifo cha uchungu msalabani,na alikubali kikamilifu kufa kulipa dhambi za ulimwengu,kulingana na mipango ya Mungu. Katika dhihirisho kuu ya rehema na neema ambayo ulimwengu umewahi kushuhudia,maisha na kifo cha Yesu yalikuwa nafasi kwa wote waliomwamini. Yule asiye na makosa alikufa kuwaokoa waliokuwa na dhambi na shetani.

Lakini,kaburi halingeweza kumzuia Yesu. Baada ya siku tatu,Yesu alitoka kwa kaburi na akatimiza lengo lake humu ulimwenguni la kushinda dhambi kwa kufa msalabani na kushinda kifo kwa kufufuka kutoka kwa wafu-jinsi ambavyo Mungu aliahidi. Baada ya siku arobaini,alirudi mbinguni ambapo anatawala ama mfalme wa haki.

Lakini hadithi haiishi hapo…

1 Petro 3:18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi,mwenye haki kwa ajili yao waio haki ili atulete kwa Mungu.
Wagalatia 1:4 Kristo ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa kama alivyotenda Mungu Baba yetu.
KILA KITU KIPYA

Kwa wote wanaomwamini Kristo pekee,Mungu pia ameahidi kwamba atafanta mambo kuwa mapya. Mbingu mpya nan chi mpya hazitakuwa na dhambi na uchoyo-mahali pa ibaada kamili na Mungu,watu wengine na viumbe vyote. Hakutakuwa na mitetemeko ya ardhi,vimbunga au hata mafuriko makubwa ambayo yataathiri ulimwengu. Hakutakuwa na machungu,mioyo iliyovunjika,magonjwa au hata kifo vya kutusumbua.

Kila kutu kitarejeshwa jinsi kilivyotakikana kuwa. Nchi mpya itakuwa nyumba kamili ambayo Mungu alitaka iwe kwa viumbe vyake. Mpango wa awali wa Mungu utaimarika na wale watakaoamini wokovu wake wataingia katika lengo kuu la kumwabudu kwa kumpenda,kumtumikia na kufurahia uhusiano naye milele.

Ufunuo wa Yohana 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
MILELE NA MUNGU

Jambo la kufurahisha kuhusu dunia mpya ni kwmaba, tutakuwa na Mungu milele tukiwa na furaha. Tutarejeshwa kwa uhusiano kamili na Yule aliyeumba, aliyependa na kufa kwa ajili yetu. C. S. Lewis ambaye ni msomi mkuu na mwandishi wa vitabu vya watoto alilinganisha hatua ya kwanza ya kuingia katika dunia hii mpya na “Sura ya Kwanza ya Hadithi kuu ambayo hamna mtu duniani amewahi kuisoma; ambayo yaendelea milele; na kila sura ni nzuri kuliko iliyoitangulia.”

NI IPI SEHEMU YAKO KATIKA HADITHI?

Mungu anaandika hadithi ya kushangaza kutoka wakati wa uumbaji hadi urejesho. Alikuumba ili uwe sehemu ya hadithi ya kumwabudu,kumtumikia na kufurahia uhusiano naye. Kwa kuungana na Mungu katika hadithi hii,utapata msamaha,lengo na kutosheka unapomjua Mwandishi wa maisha.

WOKOVU KWA IMANI PEKEE

Imani ni kumwamini Yesu Kristo pekee ambaye anaweza kukuokoa. Yamaanisha,badala ya kuamini kwamba waweza kujiokoa kutokana na athari za dhambi,waweka imani hiyo kwa wokovu aliokununulia kwa kifo chake. Uaminifu wako ni kwa Yesu,Mfalme. Wale wanaoweka imani yao kwa kitu kingine isipokuwa Yesu watajipata wametengwa kwa Mungu wa upendo aliyetupa mwanawe wa pekee atuweke huru kutokana na mzigo wa dhambi. Kutenganishwa huku kwa machungu kwaitwa Jahanamu.

Waefeso 2:8–9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu,ni kipawa cha Mungu;wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu.
JIBU

Mungu anakualika kuwa sehemu ya hadithi ambayo anaandika kwa vizazi vitakavayokuja. Anakupa wokovu leo ambao ni mwaliko wako kwa wokovu ambao Mungu anakupa. Waweza kukumbatia wokovu wa Mungu kwa:

KUKUBALI UNAMUHITAJI MUNGU
MUOMBE AKUSAMEHE
KUMWAMIZI YESU PEKE YAKE AKUOKOE
KUMFUATA YESU KRISTO, MFALME WA MAISHA YAKO, KWA IMANI KUANZIA SIKU YA LEO NA ZIJAZO

Wakati unapomwamini Yesu Kristo, unakuwa MWANA wa Mungu na roho wake anaanza kuishi ndani yako. Umekuwa sehemu ya hadithi yake. Unapozidi kukua katika uhusiano na Mungu, unazidi kuona na kuelewa hadithi yake maishani mwako. Dhambi zako zote, za zamani, za siku za usoni zimesamehewa na utapata kukubalika kabisa mbele zake. Unapoanza uhusiano huu, Yesu aahidi kuwa nawe kwa mazuri na mabaya na changamoto za maisha haya. Anakupenda na upendo usiobadilika wa milele. Na hajaahidi tu uzima wa milele, lakini alikuja ili uweze kukumbana na lengo, maazimio na uhuru wa maisha haya.

Yohana 6:47 Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
Skip to content